الأربعاء، 22 أبريل 2009

NADHARIA YA TAKWIMU YA LUGHA YA KUDURUSU MTINDO

NADHARIA YA TAKWIMU YA LUGHA YA KUDURUSU MTINDO


Hakika nadharia ya takwimu ya lugha ya kusoma mtindo unaweza kudurusu mitindo yoyote mtazamo unaotiliwa mkazo na mtafiti, kati ya mambo ambayo nadharia ya takwimu inajengwa juu yake ni kwamba matini ya fasihi kwa mtunzi maalum au katika elimu ya kifasihi maalum ina baadhi ya mambo muhimu yanayohusiana na lugha, kati yake ni:

1-Utumiaji wa mambo yanayofanana na maneno yaliyokuja ndani ya kamusi.
2-Kuongeza au kupunguza katika kutumia baadhi ya maneno maalum.
3-Urefu wa sentensi au ufupi wake.
4-Urefu wa maneno yanayotumiwa au ufupi wake.
5-Aina za sentensi (sentensi ya jina –sentensi ya kitenzi)
6-Athari ya mpandano wa maneno au vinyume na kuazima maneno maalum.

Kwa ufupi tunaweza kusema kwamba ufahamu wa mtindo kutokana na nadharia iliyotangulia inahusiana zaidi na maana ya kutohakikisha(intimali).
Masomo ya kimtindo yanatumia njia ya kukusanya nyanja kadhaa tunataja baadhi yake kama:

1-Usaidizi katika kuchagua aina kwa kuzichagua uchaguzi nyeti pale ambapo zinahusiana jamii inayotakiwa kusoma.

2-kupima kuzidi kwa sifa za kimtindo katika kazi mahususi, basi tunapotaka kupima kuzidi kwa sentensi ya jina katika matini mahsusi tunasimama kwa kupima idadi ya sentensi iliyokaririwa, kisha tunaigawanya juu ya urefu wa matini kutokana na idadi za sentensi ndani yake.

3-kupima kiasi kati ya idadi ya kutaja kwa sifa maalum ya kimtindo na idadi ya kutaja kwa sifa nyingine kwa ajili ya kulinganisha kati yao na njia hiyo inayofanywa kwa kugawanya kwa kukusanya idadi ya maana za kutaja kwa mojawapo zaidi ya sifa nyingine na kwa njia hiyo tunaweza kuhesabu nisba ya sifa nk.




Mtunzi anajaribu katika nadharia hii kutoa jambo jipya juu ya msingi wake inaweza kutenganisha (kupambanua) baina ya mitindo kwa mfano:

1-Kutenganisha baina ya lugha ya fasihi na lugha elimu.
2-Kutenganisha baina ya lugha ya ushairi na lugha nathari
3-Kutenganisha kwa lugha zinazotumiwa kupitia aina za kifasihi.

Na mwisho wa lengo lililokusudiwa, na mwana elimu wa Ujerumani Busemann ni kwamba inawezekana kupambanua kwa matini ya kifasihi kwa kuainisha kwa nisba baina ya kueleza kwa tukio (vitenzi) na kueleza kwa kutumia sifa kwa kukusanya idadi ya vitenzi katika matini na idadi ya sifa, na matokeo ya njia hii ni kujua kwa idadi ambapo huenda zikazidi au zikapungu kwa mujibu wa kuongeza au kupunguza idadi ya vitenzi juu ya idadi ya sifa. Nisba hiyo inatumia kwa kuzingatia kama ni dalili ya juu ya ufasiri wa mtindo, na kama nisba hiyo imeshaongezwa ilikuwa mtindo wa lugha ni karibu zaidi na mtindo wa kifasihi na inapopunguzwa itakuwa mtindo ni karibu zaidi na mtindo wa kielimu na njia ya Busemann kama yafuatayo:

Nisba ya kitenzi kwa sifa =idadi ya vitenzi ÷ Idadi ya sifa

Na njia hii inafupishwa ( N T S ) pale ambapo
N=kiwango T=kitenzi S= sifa, na ngeli ya vitenzi inakusanya vitenzi vyote isipokuwa vitenzi visaidizi. Na ngeli ya sifa inakusanya maneno yote yanayokuja kama ni fasihi katika kuzungumza ( sifa + yanayosifiwa ) na inakusanya pia maneno yanayotenda kazi ya sifa.

Na katika matokeo ambayo mtunzi amewasili kwake kwa methodolojia yake ya kilugha ni:

1-Unaweza kupambanua kwa jinsia ya mtunzi kama ni mwanaume au mwanamke.

2-Unaweza kujua umri wa mtunzi kama ni kijana au mzee (sheikh).

3-Unaweza kurejesha matini zisizo na mtunzi kwa mwanzo wake.

4-Kupambanua kati ya amali ya kifasihi na amali ya kisayansi.


(Aina za mitindo)

Maulamaa wamejitahidi katika kugawanya mitindo ya lugha na madhehebu yao yamekuwa mbalimbali katika kuigawanya kutokana na maono yao.

Baadhi yao wamegawanya mitindo kwa upande wa mtazamo wa kilugha kama mitindo ya sharti, ulizo n.k. Kutokana na mitindo ya kilugha.

Baadhi yao wamegawanya mitindo kwa upande wa mtazamo wa kilugha kama mitindo ya tashbihi, kina ya istiana n.k.

Na baadhi yao wamegawanya mitindo kwa upande wa kazi zao kama mitindo inayohusiana na maisha kwa mfano mitindo ya miamala ya watu , mitindo ya kielimu na ya kijamii.

Na baadhi yao pia wamegawanya mitindo kwa upande wa mitazamo ya kifasihi kutokana na malengo ya mwandishi, kwa mfano mitindo ya kisa, makala n.k.

(Mitindo ya kikazi)

(Nadharia ya mitindo ya kikazi kama ilivyokuja na, BARTH 1969).

Nadharia hii inafahamisha kwamba nidhamu yoyote ya kilugha ina malengo yanayofanana lakini malengo hayo yanagawanyika kutokana na mambo yanayoashiria mazungumzo kwa mfano, shughuli ya mawasiliano inaitwa mtindo wa mazungumzo n.k.
Na matokeo ya hayo yaliyotangulia tunakuta kwamba mitindo ya kilugha ambayo mtu anayatumia yanabadilishwa kama maudhui ikibadilishwa kwa upande mmoja na wanaoshiriki katika mazungumzo au wasikilizaji wake kwa upande mwingine, mitindo inageuzwa vile vile na vipengele vingine, baadhi ya vipengele hivyo ni vipengele vya jamii, kisaikolojia au vyote viwili, vilevile mitindo yanatofautina kutoka na aina ya kifasihi ambayo mwandishi anaizungumzia, pia mwandishi ana umuhimu mkubwa katika kutofautisha mitindo.
Masomo ya kilugha yamebainisha kwamba mitindo tofauti ni matokeo kwa hali ya kijamii mahususi, wanafalsafa wanaiita (sharti ya kijamii), yaani kila mtindo ni tokeo la kijamii una sifa za kijamii zenye malengo mengi na tofauti. RIEZEL amepambanua kati ya kazi tano za kimtindo kutokana na kazi zake za kijamii nazo ni:

1-Mtindo wa miamala wa kinasimu kwa mfano, balagha, hadithi za kinasimu na kanuni.
2-Mitindo ya kielimu kwa mfano, mihadhara ya kielimu na ya kisanaa.
3-Mtindo wa magazetini na uchapishaji, na kati yake maoni ya wanahabari na ukosoaji wa habari.
4-Mtindo wa miamala ya kila siku na humathilisha (kufananisha) katika mazungumzo ya watu na mawasiliano yao wenyewe kwa wenyewe.
5-Mtindo wa sanaa nzuri unamathilisha katika matini za kifasihi.

MARTIN JOOS ameongeza aina mbili za mitindo ya kikazi katika aina zilizotangulia nazo ni:

1-Mtindo wa ushauri utumiao kati ya hakimu na washauri wake au mawaziri wake wakati wa kujadili kuhusu mambo ya dola.
2- Mtindo wa upendo na malengo yake ni kuzungumza zaidi juu ya yaliyo ndani ya moyo kama mapenzi, na mtindo huo ni mtindo utumiao kati ya mume na mke (wanandoa) na wanaoishi katika familia moja.

Na katika nyanja ya lugha ya Kiswahili MAW.J mwaka 1974 amegawanya mtindo wa nathali ya Kiswahili katika:

1-Mtindo wa maneno yaliyosemwa. Na mtindo huo una baadhi ya sifa kama kuzitumia sentensi zenye urefu au ufupi, kukithiri kwa kutumia viambishi vya kurejea na kutumia vivumishi vya kuonyesha kabla ya jina.
2-Mtindo wa maneno yaliyoandikwa na mtindo huo una idadi kadhaa za vipengele vya kilugha katika ibara ya sentensi wastani.

MAW.J amegawanya mitindo ya nathari kwa ujmla katika mitindo mine:

1-Mtindo wa kwanza:
Mtindo wa munadhama na mtindo huo una baadhi ya sifa kama kuzidisha idadi za vipengele vya kitenzi juu ya vipengele vya kijina.

2-Mtindo wa pili:
Mtindo wa kukamilisha na mtindo huo una baadhi ya sifa kama setensi zenye ibara mmoja na kuwepo kwa vipengele vya kijina kwa uwazi.

3-Mtindo wa tatu:
Mtindo wa visa na mtindo huo una baadhi ya sifa hasa kama kuwepo ibara tofauti pamoja na ongezeko la nisba ya ibara ya kitenzi na kutumia kwa vivumishi vya kuonesha na vivumishi vya kumiliki kabla ya jina.

4- Mtindo wa nne:
Mtindo wa mazungumzo unaotambuliwa kwa ibara zake zilizofungamana na sentensi zake fupi na tamko lenye neno moja.

Kwa hivyo tunaona kwamba MAW.J amegawanya mitindo kwa upande wa kazi zake kutokana na maudhui ambayo mwandishi au msemaji anazungumzia juu yake, na kwa kuangalia tunaona kwamba yeye ameegemea katika uchunguzi wake juu ya kutafsiri kwa kilugha na upande wa kifasihi haukuwa na nasibu (sehemu) yoyote katika uchunguzi huo.

Na kwa upande mwingine MWANSOKA 1991 ameigawa mitindo katika lugha ya Kiswahili, katika vigawanyo vinne vya kazi navyo ni:

1-Mtindo wa kitaaluma:
Unahusisha na mtindo wa vitabu vya shule, majarida mahususi,mtindo wa mihadha ya chuo kikuu, vikao vya uchunguzi, ripoti na ujumbe wa kielimu .

2-Mtindo wa kirasmi:
Unahusisha na mtindo wa mazungumzo kazini, mikutano ya kidiplomasia, kanuni, mikutano na uamuzi wa kiserikali

3-Mtindo wa magazeti na shughuli za kisiasa.
Unahusisha na mtindo wa majarida ya kitaifa na ya kichama, majadiliano ya bunge na mikutano ya chama.

4-Mtindo wa mawasiliano ya kawaida (yasiyo rasmi).
Uhusiano na mtindo wa maisha ya kila siku baina ya watu na nyumbani na baina ya wasafiri na marafiki.

Kutokana na migawanyo hiyo ya kikazi tuliyotanguliza kwa mitindo tunatoka kwa mgawanyo wa kikazi kwa mitindo inayojegwa juu ya yaliyotangulia nayo ni:
1-Mtindo wa kirasmi. 2-Mtindo wa magazeti.
3-Mtindo wa kishauri. 4-Mtindo wa kitaaluma.
5-Mtindo wa miamala wa kirasmi 6-Mtindo wa fasihi nzuri.
kutokana na migawanyo ya mitindo kwa upande wa kazi, tunaleta miganyo ya mitindo kwa upande wa fasihi, nayo ni.

(Mitindo ya kifasihi)

Mtindo wa mtazamo wa lugha ya fasihi juu ya lugha inayoandikwa au fasihi tu, bali unafungamana na sharti la jamii kwa mujibu wa hitilafu ya tabaka za kijamii na utamaduni zinazohitilifiana.

Ni wajibu kuuliza juu ya mtindo wenye methali ya kifasihi, je faida na sifa za kueleza zinakuja katika methali ya kifasihi zinakwenda sambamba pamoja na mitindo au la?
Hakika lugha ya kifasihi inakwenda kinyume na lugha ya mawasiliano ya kila siku nayo ni yenye kufahamika zaidi na yenye kukusudiwa katika kujengwa kwake, kwani fasihi inatumia lugha utumiaji mzuri sio wa mawasiliano.
Na hiyo inatuelekeza kwa kuonesha migawanyo ya mitindo kwa upande wa kifasihi kwani kutofautiana kwa mitindo ya kifasihi kunarejea kwa sababu mbili:

Ya kwanza: maudhi
Nayo ni fani ya kifasihi ambayo mwandishi anachagua kwa ajili ya kueleza kwa yaliyo ndani yake na kwa upande wa elimu,fasihi, shairi na nathari, basi kila moja kati yake ina mtindo wake mahususi ambao hujulikana kwake na kwenda sambamba pamoja na tabia yake ya kifasihi.


Ya pili: mwenye fasihi.
Hitilafu ya mtindo hapa inarejea kwa hitilafu ya akili za wenye fasihi, tabia zao na njia ya fikra zao na Dokta,Ash shayb (1939) amegawanya mitindo kwa upande wa kifasihi katika mtindo wa kielimu na mtindo wa kifasihi, na amegawanya mitindo ya nathari katika migawanyo miwili.

Ya kwanza: Nathari ya kielimu.
Nathari hiyo ina sifa zake zinazoitambulisha na inachukuliwa kama njia ya kueneza maarifa, na maarifa ya kiakili ni msingi wake na mara chache unakuta athari ya ghadhabu ndani yake.



Ya pili: Nathari ya kifasihi.
Nathari hiyo inatambuliwa kwa kuingiza hisia ndani yake pamoja na kuingiza hakika na fikra zenye umuhimu zaidi nayo ni lugha ya hisia na lengo lake ni kuchochea kwa hamasa katika nafsi za wasomaji na wasikilizaji.

(Mtindo wa maisha ya kibinafsi)

Ama mtindo wa maisha ya kibinafsi ambao uchunguzi unakuwa juu yake, basi Dk Ash shayb ameijaalia katikati baina ya mtindo wa kitaaluma na mtindo wa kifasihi, basi ikiwa mtindo wa maisha ya kibinafsi unakutwa ndani yake mtindo wa kitaaluma na kifasihi,basi kwa nini usiwekwe mgawanyo mwingine wa mtindo ambao unakusanya kati ya mitindo miwili ya kitaaluma na kifasihi? Nasi tuna mtindo unaoumathilisha nao ni mtindo wa maisha ya kibinafsi.

Na maisha ya kibinafsi ambayo Dk Abdul-Aziz Shah ameiita kwa jina la maisha ya kibinadamu amezigawanya baadhi katika migawanyo miwili.

Maisha ya wengine:
Nayo ni utafiti juu ya hakika katika maisha ya mwanadamu hodari na kuchambua kwa uhodari wake,siri zake au siri za uhodari wake toka katika hali ya maisha yake na matukio aliyoyakubali na athari aliyoiacha katika rika lake.

Maisha ya kibinafsi:
Mwandishi mwenyewe anaandika maisha yake ya kibinafsi hali ya kufichua pia siri za maisha yake ya ndani na kutazama kwa makini kwa nafsi yake inayojumlisha kwa kuwepo utajiri wa ndani, na sifa zinazojaalia maisha ya kibinafsi ni kubwa sio sifa zinazojaalia maisha ya wengine kuwa ni kubwa. Na sifa kuu kati ya sifa hizo ni kuwa mwandishi wa maisha ya wengine, ana mtazamo wa maudhui anatambua kwa haraka,anafahamu kwa makini na anajua uhakika wote na anatoa hukumu juu yake.
Ama mwandishi wa maisha ya kibinafsi naye ana ubinafsi kabla ya kila kitu naye anatazama nafsi yake kwa uangalifu.
Dk Ash Shayb anasema kwamba maisha ya kibinafsi yanahesabu historia inayohusiana na maisha ya watu na mpango wake unafuata njia tatu.


Ya kwanza: Mwenye historia anaandika katika maisha ya mwingine, basi anachagua matukio na athari na anazipanga na anazifasiri.

Ya pili: Mwenye historia anachagua njia isiyo ya moja kwa moja naye anaficha nyuma ya maudhui ili ajaalie aoneshe nafsi yake,basi anatuonesha maneno ya mtu, maoni yake, madhehebu yake ya tabia,marafiki zake, wanafunzi wake, mashairi yake na athari yake bila ya kuzungumza kwa kuzikosoa na kuzichambua.

Ya tatu: Mwenye historia anaandika maisha yake mwenyewe kwa kalamu yake, basi anzungumzia juu ya hakika na anafasiri matukio aliyoyapita kwa upande wa mtazamo wake mwenyewe.

Na yaliyotangulia yanaonesha kwetu kwamba mtindo unagawanywa ima kwa njia ya kazi yake ya kijamii au kwa njia ya fani ya kifasihi ambayo mwenye fasihi anazungumzia na inachukuliwa wakati wa kusifu mitindo hiyo, chanzo chenyewe au mwenye fasihi au yaliyozunguka kwake kati ya hali ya kijamii na uwezo wa mwandishi unasimama muelekeo wake wa kifasihi, utamaduni wake, enzi yake na uhusiano wake wa kijamii.

Mtindo wa maisha ya kibinafsi juu ya viwango vitatu:

1-Kiwango cha neno
2-Kiwango cha mitindo ya kilugha
3-Kiwango cha picha za kibalagha.

Na kutokana na hayo yaliyotangulia tunakuta kwamba kila mwenye fasihi ana mtindo wake maalum.

Imetimiza


Wanafunzi waliofanya kazi hiyo ni:

• Abdallah Elashry
• Ali Gabr
• Ramadam Mosa
• Ramy Adbel Salam
• Mohammed Abbas

Maana ya mtindo na nadharia zake

MAANA YA MTINDO NA NADHARIA ZAKE

Maoni mbali mbali yamekuja katika maana ya mtindo,na wanavyoni wamegawanyika kwenye madhehebu mengi.

Maana ya kwanza:
Mtindo ni njia ya utekelezaji wa maana.

madhehebu hiyo imeunganisha kati ya mtindo na njia za utekelezaji wa maana pale ambapo kila msimamo maalum asemao.
Na uhitilafu wa mitindo hapa unarejea kwenye hitilafu ya msimamo na tabia ya maudhui na uwezo wa mwandishi wa kisanii.
Miongoni mwa wafuasi wa madhehebu hiyo ni Ibn Qutaibah, pale ambapo ameunganisha kati ya mtindo na lengo ambalo mwandishi anajizungumzia ndani yake, pia ameunganisha kati yake na hali ya mpokeaji na utamaduni wake.
Miongoni mwao ni Al-Baklani pale ameafikiana na Ibn Qutaibah katika kuunganisha mtindo kwa aina ya Fasihi katika njia za utekelezaji kila aina ndani yake, kutoka barua, ujumbe, shairi, nathiri na nyinginezo.
Na miongoni mwao Al-shaib, nao anaafikiana na walio mtangulia katika kuunganisha mtindo kwa sanaa ya Fasihi (Lengo la fasihi), kutokana na hayo ameigawanya mitindo kwenye mitindo yenye makala, hutuba, sira, kisa na nyinginezo.

Nadharia ya hitilafu ya kiwango cha lugha.

Nadharia hiyo inategemea juu ya hitimali kwamba usemaji wa lugha unahitalifiana kwa mujibu wa anaye zungumziwa na kwa mujibu wa aina ya uzungumzaji na maudhui yake.
Mfano wa hilo, mazungumzo ya kitaalamu au ya kisanii inahitilifiana na mazungumzo ya mpira wa miguu.
Nadharia hiyo ina uwezo muhimu katika tafsiri ya matini, nayo inaamiliana na maneno ya kilugha yaliyomo ndani ya kamusi ambayo ni maneno makhususi kwa mujibu wa hitilafu ya kiwango cha kilugha.
Lakini nadharia hiyo katika wakati ule ule inasisitiza juu ya kitamko zaidi ya lugha ya kimaandishi, na hakuangalia kwenye miundo ya kinahau kwa umbo la kijumla.



Maana ya pili:
Mtindo ni kuchagua kwa miundo ya kilugha na kuunga baina yao katika matini.

Kuchagua katika mtindo ni kuchagua kwa mwandishi kwa neno fulani pasipo na lingine kwani neno hilo ni karibu zaidi kwa maana au mwandishi anapendekeza neno au maumbo ya kinahau kwani umbo hilo ni sahihi zaidi kinahau na kimaana.
Ama kuunga ni kujaribu kuunga baina ya maneno ndani ya sentesi kwa ajili ya kufikia maana inayotakiwa kwa makini na uwazi.
Na kwa maana hiyo tunakuta kwamba mtindo -katika madhehebu hiyo-inachunguzwa kupitia kwa matini ya maandishi tu pasipo na kushughulika kwa mwandishi au anayepokea.
Miongoni mwa wafuasi wa madhehebu hiyo ni Abdul-khahir Aljirjaniy.
Maneno yake ya mwisho kwamba mwandishi anachagua maneno ndani ya nafsi yake na anayewafikiana na maana anazipanga maana ndani ya nafsi yake na anaziweka kwenye umbo sahihi la kinahau na anajenga baadhi yake juu ya baadhi nyingine kwa ajili ya kuonyesha juu ya fikra anayeitaka. Abdel kaher amejaaliwa kuchagua kwenye lafudhi (maneno) na kuunga baina ya maneno kwa ajili ya kupata fikra sahihi anayotaka kueleza na anajalia mtindo anakusanya lafudhi na maana, kuchagua kunakuwa kwenye lafudhi na kuunga katika maana.
Na miongoni mwao Ibn Khaldon amesisitiza juu ya lafudhi kwani ni zinabainisha maana inayotakiwa kwani maana inapatikana katika lafudhi, na uwezo wa mwandishi katika kuzichagua lafudhi kwa njia sahihi na kuunga baina yao ni ambazo zinavuta kwa maana ya kina zinazokusudiwa na hapa tunamkuta ameafikiana na Abdel Kahr katika kuchagua na kuunga baina ya lafudhi pamoja na kulazimika na mahusiano ya kinahau baina yake.

Maana ya tatu:
Mtindo ni mtu.
Maana hiyo inategemea juu ya maisha ya mtungaji, sera zake mwenyewe, na umeizingatia ni msingi muhimu katika uchunguzi na utafiti. Na kunashughulikiwa pia na jamii ya mwandishi utamaduni wake na majaribio yake.
Miongoni mwa wafuasi wa madhehebu hayo ni Ibn Al-athir kwani mtindo wenyewe unategemea uwezo wa mwandishi katika kueleza yaliyo ndani yake kwa njia nyingi Ibn Al-athir ameunganisha kati ya mtindo na kati ya mwandishi na uwezo wake wa kisanii, na kuutumia uwezo huo katika kuonesha fikra katika mitindo mizuri na njia mbalimbali, pale ambapo tunaweza kuiona hitilafu hii katika kuonesha fikra moja kwa waandishi wawili waliohitilifiana, kila mmoja kati yao anaitumia kwa mtindo wake maalum, au mwandishi anatoa fikra hiyo hiyo kwa njia mbali mbali.
Na miongoni mwao ni Boffun yeye amesema kwamba mtindo ni mtu. Maana hiyo inaungaisha baina ya mtindo asili yake kwa upande wa vipengele vya kisaikolojia, kiutamaduni, na kijamii. Naye anakusudia tabia ya mtungaji, uhakika wake, na ufahamu wake wa kilugha.
Naye anaelezea mtindo hapa. Kama ni njia ya mtungaji mwenyewe au mwenendo wake katika maandiko. Na juu ya maana hiyo imeundwa nadharia ya mtindo wa mtu: Nadharia hiyo imesimama juu ya msemo kwamba mtindo ni mtu. Na kwa maana hiyo tunaweza kuainisha kutokana na mtindo saikolojia ya mwandishi, upendeleo wake, matakwa yake, na muundo wa kisaikolojia, unaozifanya zana zake za kiisimu zinachukua njia hiyo au ile.
Nadharia hiyo inamtakia mtafiti wa mtindo ujuzi wa ukamilifu kwa maisha ya mtungaji, sera yake mwenyewe, jamii yake na enzi yake ya kihistoria.
Na hayo kwa kawaida inamchukua mtafiti nyanja nje ya ile anayoitafiti ndani yake. Na hayo sio rahisi kuitekeleza kwa namna njema katika muda unaokubalika. Kwa upande mwingine, mchunguzi katika nyanja ya mtindo hawezi kukaribu na matini ambayo mtungaji wake hakujulikana ili kuisomesha. Kutokana na hayo ni vigumu kuitekeleza nadharia hiyo juu ya matini ya fasihi kwa jumla.

Maana ya nne:
Mtindo ni kiongezi kizuri na ni ziada ya kuelezea.
Na ziada ya kuelezea inabainika wakati wa unganishi kati ya misemo miwili, ya kwanza ni msemo usiokuwa na kielezea na inatekeleza maana tu,
ya pili inatekelezea maana hiyo hiyo, lakini mwenyewe ameitengenezea na ameipa mifano.
Na kwa msingi huo, mtindo hapa ni kiongezi cha kielezea chenye kuathiria vipengele vya lugha kisiokuwepo hapo kabla na kinachozidi kutokana na nguvu ya maana na athari yake. Miongoni mwa wafuasi wa madhehebu hii Charle Bally, naye ameona kwamba mtindo ni kiongezi kizuri na ziada ya kielezea, na mtindo wenyewe unadhihirisha katika kundi la vipengele vya lugha vyenye uathiri wa kipenzi juu ya msikilizaji au mwandishi.






Shule ya mtindo wa kielezea

Shule hiyo inalingana na, ambayo kiongozi wake ni Sharle Bally, utafiti wa vipengele vya kielezea vilivyofichika au vilivyochochekea ndani ya maneno. Kwa mfano. Kauli yako, nenda hilo, naapa kwa mola wako nenda hilo, ni starehe na nenda hilo. Pamoja na maneno hayo yote yametekelezea kwa kitendo cha amri kilichopelekwa kwa anayesemwa wa kiume, isipokuwa vidokezo, vihushio, vinaashiria, vinadhihirisha mambo mbalimbali vya upenzi. Shule hiyo imejitenga na kutafiti katika matini ya nathiri ya kisayansi ambapo kawaida haisifika na kuwepo mapenzi ndani yake. Na utekelezo wake umeshughulikia na vitamkwa zaidi kuliko maandishi, na wala haishughulishwa na maandishi mapya ya kifasihi. Kwa hivyo haiwezekani kwa shule hiyo kutekeleza maendeleo makubwa katika utafiti wa kimtindo au utafiti ukamilifu juu ya mtindo.

My Own Room


Go Large!
بروف عباس يرحب بكم على المدونه الالكترونيه الخاصه به profabbas.blogspot.com ويرحب باستفساراتكم على الايميل الخاص به professor_abbas@hotmail.com